About
You can also join this program via the mobile app. Go to the app
5-DAY CAKE ART CHALLENGE
Jifunze mbinu za kuandika ujumbe, kuchora michoro na kuhamisha designs kwenye cake kwa kutumia icing na piping bag. Katika siku tano, utajifunza hatua muhimu za kuboresha ujuzi wako wa cake writing na cake drawing.
Essentials of Cake Art ni challenge ya siku tano iliyoundwa kukufundisha misingi na mbinu za kuandika na kuchora kwenye cake.
Utajifunza namna ya kuandaa icing yenye consistency sahihi, kutumia piping bag kwa control nzuri, kuunda michoro mbalimbali na kuandika maneno kwa kutumia mbinu za kaligrafia.
Challenge hii itakusaidia kuongeza ubunifu na kujiamini katika kupamba cake zako kwa maandishi na michoro.
Jifunze kuandaa icing yenye consistency inayofaa kwa ajili ya kuchora na kuandika kwenye cake.
Jifunze kushika na kutumia piping bag kwa usahihi, kutengeneza mistari, maumbo na sketch mbalimbali.
Jifunze kuunda herufi, kuandika maneno na kutumia mbinu za kaligrafia kuandika ujumbe kwenye cake.
Jifunze kuhamisha sketch na michoro kutoka kwenye karatasi kwenda kwenye cake kwa kutumia mbinu na vifaa mbalimbali.
Jifunze kutumia piping bag kuchora figures na michoro moja kwa moja kwenye cake.
Masomo ya video kwa siku tano.
E-book ya kukusaidia kufuatilia masomo.
Templates za kupakua na kuchapisha kwa ajili ya mazoezi.
Certificate of Completion baada ya kukamilisha masomo yote matano.
Wewe ni beginner unayetaka kujifunza cake writing na cake drawing.
Tayari unaoka cake lakini ungependa kuongeza ujuzi wa kuandika na kuchora kwenye cake.
Unafanya biashara ya cake na ungependa kuongeza huduma na ubunifu kwenye kazi zako.